Wednesday 22nd, January 2025
@Tanzania
Hayati Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ilikuwa Tanganyika). Ifikapo tarehe 14/10/2017 atakuwa anafikisha miaka 18 tangu atangulie mbele za haki huku Taifa na vizazi vyake vikiendelea na kumbukumbu ya kifo chake na kumuenzi.
Kitaifa Maadhimisho hayo huambatana na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika Mkoani Mjini Magharibi Zanzibar, Mgeni rasmi atakuwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, hata alipopingwa baadaye waliompinga walikiri ukweli wa maono yake. Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa Mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake. jambo mojawapo alilolisema julai 29/07/1985, kwamba "kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu Mimi , ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa Binadamu." Mwenyezi Mungu Mrehemu.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa