CHINI YA UONGOZI WA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UWAZI KATIKA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA WAONGEZEKA
•Akutana na Bi. Helen Clark mwenyekiti wa bodi ya EITI.
•Mkutano wa 62 wa bodi ya Kimataifa ya EITI wafanyika nchini.
•Ripoti za TEITI kutolewa kwa wakati.
•Tanzania ipo juu katika utekelezaji wa viwango vya Kimataia vya EITI. (Tathamini iliyopita ilionesha Tanzania ilipata 77/100).
i)Uwekaji Wazi wa Ripoti za TEITI
Katika kipindi cha miaka minne (4), TEITI imefanikiwa kutoa ripoti nne (4) za TEITI kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019; 2019/2020; na 2020/2021; na 2021/2022. Ripoti hizo zimefanya ulinganishi wa malipo ya kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na mapato kwa Serikali Kuu na katika Halmashauri ambazo zinapokea tozo (Service Levy) kwa mujibu wa Sheria ya Local Government Finance Act, 1982 . Ripoti hizo zinapatikana katika tovuti ya TEITI (www.teiti.go.tz).
ii)Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Samia Suluhu Hassan, alihutubia Mkutano wa Kimataifa ya EITI
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alihutubia Mkutano Mkuu wa Asasi ya Kimataifa ya EITI (EITI Global Conference) uliofanyika Dakar- Senegal. Ushiriki wa Mkutano huu kama nchi ni ishara ya uimara wa nchi katika utekelezaji wa vigezo vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Mkutano huu ulihudhuliwa na washirki zaidi ya 1,500 kutoka nchi wanachama ya Umoja wa Kimataifa Duniani.
iii)Kupitishwa kwa Muundo wa TEITI (Organization Structure)
Katika kipindi cha miaka minne (4) ya uongozi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu, Muundo na mgawanyo wa majukumu ya Taasisi ya TEITI ulipitishwa. Kuidhinishwa kwa Muundo huo kutawezesha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi kikamilifu na kwa ufanisi.
iv)Utekelezaji wa Sheria ya TEITA, 2015
Katika utekelezaji wa Sheria ya TEITA, 2015, TEITI imeongeza uwazi juu ya matumizi ya mapato ya Halmashauri yanayotokana na tozo ya huduma (Service Levy) na malipo yanayohusu wajibu wa makampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility (CSR)) kutoka kampuni za uchimbaji wa Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Aidha TEITI ipo katika hatua za mwisho katika takwa la Sheria ya TEITA, 2015 la uwekaji wazi wa Mikataba ambao Serikali imeingia na kampuni za Madini, Mafuta na Ges Aslia.
v)Uteuzi wa Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamuhuri ya muungano alimteua CPA. Ludovick Utouh kuwa Mwenyekiti wa kamati ya TEITI kusimamia shughuli za kamati ya TEITI chini ya kifungu cha tano (5) cha Sheria ya TEITA, 2015 ya utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika sekta Madini,Mafuta na Gesi Asilia.
vi)Ushiriki wa TEITI katika Uhamasisha matumizi ya takwimu zinazotolewa na ripoti za TEITI
TEITI ilishiriki na kutoa elimu kuhusu majukumu yake wakati wa Maonesho mbalimbali yakiwemo maonesho ya kimataifa ya sabasaba, nanenane na maonesho ya kitaifa ya uwekezaji katika sekta ya madini Mkoani Geita. Aidha, TEITI imeshiriki katika warsha mbalimbali kuelimisha umma juu ya matumizi takwimu zinazotolewa na ripoti za TEITI za kila mwaka katika kuhoji juu ya manufaa ya rasilimali hizo kwa wananchi na nchi kwa ujumla. TEITI imefanya warsha Mikoa ya Geita, Mwanza, Songwe, Mtwara na Lindi. Aidha kundi maalum la wananchi wasioona walihusishwa katika uhamasishaji huo.
vii)Kuratibu Mkutano wa Bodi ya Kimataifa EITI
TEITI imeratibu kufanyika kwa Mkutano wa 62 wa Bodi ya Kimataifa ya EITI uliofanyika hapa nchini tarehe 13 na 14 Machi, 2025. Mkutano huo wa Bodi ni fursa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla kwa kuwa Tanzania ilipokea ugeni wa zaidi ya washiriki mia moja ikijumuisha wawakilishi wa Makapuni Makubwa duniani yanayojihusisha na Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia hivyo ni Kivutio cha Uwekezaji katika nchi yetu, Vilevile, ni fursa ya kuongeza fedha za kigeni kwa kuwa wageni hao walitumia bidhaa na huduma hapa nchini.
viii)Ujio wa Rt. Hon. Helen Clark – Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya EITI
Katika kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi ya Umoja wa Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji na nchi ya Tanzania, mwenyekiti ya Bodi wa EITI, Rt. Hon. Helen Clark aliyetembelea Tanzania na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mawaziri wa Nishati na Madini hapa nchini lengo likiwa ni kujadili utekelezaji wa shughuli za uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini Mafuta na Gesi Asilia.
ix) TEITI imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Asasi za Kiraia, Serikali na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia katika utekelezaji wa masuala ya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kulingana na Sheria ya TEITA, 2015.
x)Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za EITI hapa nchini
TEITI ilifanyiwa Tathmini (validation) ya utekelezaji wa shughuli za uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia na Bodi ya Asasi ya Kimataifa ya EITI. Matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa Tanzania imepata daraja la moderate (Daraja la tatu) katika kutekeleza vigezo vya EITI vya mwaka 2019 ambapo Tanzania imepata alama 77/100 kwa kuzingatia maeneo matatu ambayo ni Stakeholder engagement (82.5), Transparency(73.5) pamoja na Outcome and impact (75.5). Bodi hiyo imepongeza juhudi za Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli za EITI hapa nchini.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.