*MAKALA*
IJUE DHANA YA VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI
Kwanini Madini ni Maisha?
Vision 2030 inabebwa na dhana nzima ya umuhimu wa madini katika maisha ya kila siku ambapo uwepo wa madini na miamba ya madini unagusa maisha ya kila mtu. Kuwepo kwa madini, kunawezesha watu kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kujiingizia vipato vya moja kwa moja na vipato vingine vinavyotokana na shughuli za biashara kama za chakula ikiwemo za utoaji huduma, usambazaji wa vifaa vinavyohitajika kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji madini.
Kwa kuzingatia hayo, Sera ya Madini ya mwaka 2009 imesisitiza juu ya kufungamanisha madini na sekta nyingine hivyo, Vision 2030 inalenga kuboresha maisha ya watu kupitia sekta mbalimbali.
Kama inavyofahamika duniani kote, uchimbaji wa madini huwa na tija endapo ukiendeshwa kisayansi, hii inapunguza upotevu wa mitaji na uhifadhi wa mazingira kwa kufuata maeneo yenye rasilimali madini pekee. Kwa Tanzania, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ndiyo mzalishaji wa taarifa za awali za jiosayansi ambazo zinatoa mwongozo wa mahali yalipo madini na aina yake katika sehemu mbalimbali nchini. Jambo hili ni muhimu sana kwa wachimbaji wadogo na wakubwa Tanzania kama ilivyo kwenye nchi nyingine zenye shughuli za uchimbaji wa madini zilizoendelea.
Kwa Tanzania, GST ndiyo inajua jiolojia ya nchi na ni muhimu sana kutumia taarifa zao ili kupata mwongozo katika kuendesha shughuli za uchimbaji. Kwa mfano, migodi mingi iliyoanzishwa nchini ikiwemo ile ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na Bulyanhulu ilianzishwa kutokana na taarifa za tafiti za miaka ya nyuma za GST. Pamoja na hiyo, hata migodi inayotarajiwa kuanza kama ile ya Kabanga Nickel ni kazi zilizofanywa na GST kipindi cha nyuma mnamo mwaka 1978.
Hivyo, ili kuwepo na manufaa zaidi ya Sekta ya Madini kwenye uchumi na maendeleo ya nchi ikiwemo kuchangia zaidi ya asilimia 10 ya mchango wa Sekta ya Madini katika pato la taifa,Serikali inakusudia kuiwezesha GST kuzalisha taarifa za kina kupitia tafiti za jiofizikia (High Resolution) kupitia Vision 2030 ambazo zitavutia uwekezaji kwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
isome zaidi www.madini.go.tz
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa