KAMISHNA WA MADINI AWASILISHA MADA KATIKA KIKAO CHA UTANGULIZI KUELEKEA MKUTANO WA 62 WA BODI YA KIMATAIFA EITI
Madini Mkakati ‘’Critical Minerals”
ARUSHA
Kamishna wa Madini
Dkt. Abdulrahman Mwanga
leo tarehe 12 Machi, 2025 ameshiriki kikao cha utangulizi cha Bodi ya Kimataifa ya EITI kilichojadili masuala ya Madini Mkakati.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka kwenye umoja wa nchi wanachama wa Kimataifa EITI.
Lengo la kikao hicho ni kuzindua utafiti kuhusu Madini Mkakati na hatari za Rushwa zinazoweza kujitokeza katika uvunaji wa Madini hayo.
Aidha,kikao hicho kimejadili suluhisho la kisera ili kulinda Madini Mkakati kwa lengo la kuwezesha mhamo wa Nishati (Energy transition)
Akizungumzia katika kikao hicho Dkt. Mwanga alilisitiza kuwa kutokana na uhitaji wa Madini hayo muhimu duniani sambamba na ukuaji wa teknolojia ni vyema kuwepo na mkakati wa uvunaji wa madini hayo muhimu Barani Afrika ambapo mkakati huo utasadia kwa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Afrika kutengeneza mikakati yao inayoendana na mkakati mkubwa wa Dunia.
Amesema, wizara kupitia geological survey of Tanzania (GST) imejipanga kikamilifu kufanya tafiti mbalimbali za madini ikiwemo kutoa ushauri elekezi kupitia wataalumu wake, kudhibiti na kuzuia mianya yote ya rushwa.
Aidha,Kikao hicho kilihudhuriwa na CPA. Ludovick Utouh mwenyekiti wa Kamati ya TEITI pamoja na Katibu Mtendaji wa TEITI Bi. Mariam Mgaya.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.