Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini apokea Matokeo ya Rasimu ya Ripoti ya 13 ya TEITI kwa mwaka 2020/21*
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Bw. Kheri Mahimbali amepokea rasimu ya Matokeo ya Ripoti ya 13 ya TEITI kwa mwaka wa fedha 2020/21 iliyoandaliwa na Mtaalam Elekezi- M/S Chuo Kikuu Mzumbe. Mtaalam elekezi alieleza kuwa, ripoti imelinganisha Kampuni 45 za Madini, Mafuta na Gesi Asilia pamoja na kampuni zinazotoa huduma katika Sekta za Uziduaji.
Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Bw.Ludovick Utouh ameshukuru Viongozi wa Wizara ya Madini Waziri Mhe. Doto Biteko (Mb), Naibu Waziri Mhe. Steven Kiruswa, Katibu Mkuu Bw. Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Bw. Msafiri Mbibo kwa ushirikiano wanaotoa katika utekelezaji wa shughuli za taasisi ya EITI.
Pia, Kaimu Katibu Mtendaji Bi Mariam Mgaya alieleza kuwa ripoti ya TEITI pamoja na mambo mengine imeweka wazi taarifa mbalimbali zikiwemo taarifa za kimazingira katika sekta ya uziduaji, uwajibikaji wa kampuni kwa Jamii, na taarifa za ushirikishwaji Wazawa katika sekta ya Uziduaji.
Mwisho Katibu Mkuu Bw. Mahimbali aliipongeza timu ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa kazi kubwa ya maandalizi ya ripoti hiyo kikamilifu na kuitaka Sekretariati kuhakikisha ripoti hiyo inakamilika kwa wakati Kulingana na Matakwa ya Kimataifa ya EITI ripoti kwa kuwekwa wazi ifikapo tarehe 1 Julai 2023. Ripoti hii ya TEITI ya 13 kwa mwaka 2020/21 sasa inapatikana rasmi kwenye tovuti ya TEITI kupitia https://www.teiti.go.tz/storage/app/uploads/public/649/f22/878/649f2287817b7846038778.pdf
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa