Kuelekea kilele cha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani 2025
WANAWAKE TEITI WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA USULINI DODOMA
Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, leo Machi 06, 2025, watumishi wanawake kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) wamefanya ziara ya kutembelea kituo cha watoto yatima na wenye uhitaji kilichopo Mipango jijini Dodoma.
Kituo hicho kilichopo Mipango jijini Dodoma kilianzishwa mwaka 1995, kinahudumia watoto takribani 90, wakiwemo wale wanaohitaji msaada wa malezi bora na kukabiliana na ukatilia dhidi ya watoto
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wanawake wa TEITI, Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu, Mageni Sagenge amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yenye kauli mbiu isemayo “Wanawake Wasichana 2025 Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”, itakayofanyika kitaifa tarehe 08, Machi 2025 ambapo yataadhimishwa jijini Arusha na Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi hao wanawake wa TEITI wameamua kutembelea kituo hicho na kufanya matendo ya huruma kama vile kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali na kuwatia moyo.
“Tunatambua kila mtu ana mahitaji mbalimbali lakini nashukuru kwa michango iliyotolewa na TEITI kufanikisha jambo hili la kufanya matendo ya huruma katika kituo chetu hiki cha Usulini, jukumu la kulea watoto ni zito na linalohitaji uwajibikaji wa pamoja, hakika mnafanya kazi ya Mungu nawatia moyo japo kuna changamoto Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mama yetu Dkt. Samia Hassan Suluhu ipo pamoja nanyi kuhakikisha kuwa mnapata huduma stahiki na vituo hivi zinasonga mbele” amesema Segenge.
Ameendelea kusema kuwa, “ Natoa wito kwa wanawake wengine kuwa sisi kama walezi tunategemewa na tuendelee kuwasaidia watanzania wenzetu wenye mahitaji zaidi lakini wanakosa msaada, ambapo kutoa ni akiba ya baadae pamoja na familia zetu.”
Awali, kwa upande wake, Mlezi Mkuu wa kituo hicho Sista Maria Peter amewashukuru wanawake wa TEITI kwa umoja huo na kusisitiza wanawake wengine kujitokeza kujitolea haswa katika kipindi hichi cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.
Ameongeza kuwa mafanikio ya kituo hicho kimefanikiwa kulea watoto hadi kufikia hatua ya vyuo na vyuo vikuu.
Sista Maria ameushukuru uongozi wa TEITI kwa jambo walilofanya la kuwapatia msaada na kuongeza kuwa imewatia moyo na kujiona wa thamani sana katika jamii.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa