Teiti yahudhuria Mafunzo ya kujengea uwezo Wataalam katika masuala ya Madini Muhimu (Critical Minerals) , Jijini Nairobi, Kenya.
Mafunzo haya yameendeshwa na Serikali ya Marekani kupitia U.S. Department of State Bureau of Energy Resources kuanzia tarehe 28-31August, 2023 kupitia mwaliko kutoka Wizara ya Madini.
Mafunzo yalijikita zaidi katika Jiolojia , njia za utafiti na mifano halisi ya madini muhimu na nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa madini muhimu na umuhimu wake kwa dunia . Aidha,Wataalamu walijengewa uwezo juu ya mifumo ya Sheria na Sera zinazosimamia madini muhimu kwa kutumia mifano ya nchi zilizofanikiwa kuanzisha mipango na mifumo ya sheria katika usimamizi wa madini muhimu. Vilevile, wataalam walijengewa uwezo wa njia za ukusanyaji na uchakataji na utunzaji wa taarifa za madini muhimu kwa ajili ya kuvutia uwekezaji na kusaidia Serikali katika kufanya maamuzi.
Mjiolojia na mshauri wa masuala ya kitalaam wa TEITI, Bw. Ezekiel Seni ameeleza kuwa, mafunzo haya yamekuja kwa muda muafaka kwani tutatumia ujuzi huu kusaidia Serikali katika kuandaa mifumo ya Kisera na Sheria na kuwa na kanzi data na kuhamasisha uwazi katika hatua zote za uvunaji wa madini muhimu na mkakati (Critical and Strategic Minerals). Wataalam waliohudhuria ni kutoka nchi ya Tanzania , Marekani, Kenya na Ghana.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa