Mashirikiano baina ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji (TEITI) na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)
Timu ya wataalam wa TEITI Sekretariati ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji Meneja wa Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji Eng. Joseph N. Kumburu tarehe 14 Juni, 2023 wamekutana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kujadili maswala mbalimbali juu ya utekelezaji wa shughuli za Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia pamoja na mashirikiano baina ya Taasisi hizo.
Akielezea lengo la kikao hicho Eng. Joseph N. Kumburu amesema kuwa ushirikiano baina ya TEITI na GST utakuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji na ufanisi wa kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hizo mbili kwani dhana na dhamira kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata uelewa juu ya kazi za utafiti zinazofanywa na Taasisi GST na kuwekwa wazi na TEITI kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria ya TEITA ya Mwaka 2015.
Aidha, Mtendaji Mkuu wa GST amesema kuwa Taasisi yake ipo tayari kushirikiana na TEITI katika kuhakikisha taasisi muhimu za utafiti wa madini zinatolewa kwa waananchi sambamba na utoaji wa elimu kwa wadau mbalimbali ili kufikia lengo na dhamira kuu ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi na wadau wanapewa elimu ya kutosha kuhusiana na utafiti wa Madini na Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Madini.
Mtendaji Mkuu wa GST alieleza kuwa “GST iko tayari kupokea ushauri wowote kutoka TEITI na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuwezesha Sekta ya Madini, kupitia Taasisi ya GST inashiriki kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Mkuu Mtendaji wa GST emerizishwa na shughuli zinazofanywa na TEITI za kutoa ripoti kwa umma kila mwaka na kuahidi kuwa GST iko tayari kushirikiana na TEITI kwa kuwapa elimu watendaji wa TEITI kuhusu masuala ya utafiti endapo itahitajika. Pia, alishauri kuwekwa kwa mkakati wa pamoja baina ya Taasisi zote mbili wenye lengo la kujitangaza na kuelimisha umma wadau wa Tasnia ya Madini kuhusu masuala ya Uwazi na Uwajibikaji katika tafiti za Madini .
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa