MBIBO ASISITIZA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUJITUMA
Awataka Watumishi TEITI kutekeleza majukumu ya Taasisi kikamilifu
Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Msafiri Mbibo amewataka watumishi wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kutekeleza majukumu ya Taasisi kikamilifu.
Mbibo ameyabainisha hayo leo Mei 30, 2023 katika kikao hicho baada ya kukutana na kuzungumza na watumishi wa Taasisi hiyo katika Ofisi za Wizara Kikuyu Jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine, Mbibo amesisitiza watumishi wa Taasisi hiyo kujiamini, kufanya kazi kwa weledi, kuwajibika ipasavyo na kuwa na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kikamilifu na kuleta matokea chanya kulingana na takwa la kisheria ya mwaka 2015 TEITA-Act inavyoelekeza.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI Bi. Mariam Mgaya amewasilisha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya sasa na mpango wa bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 ambapo ameeleza kuwa kwa sasa TEITI ipo katika maandalizi ya ripoti ya 13 kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.
Kikao hicho kilihudhuriwa na watumishi mbalimbali wa TEITI pamoja na watumishi wa Wizara ikiwa ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Wizara ya Madini Bw. Nsajigwa Kabigi.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa