Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela amesema, Serikali imepelea shilingi bilioni saba kwa ajili ya kufikisha nishati ya umeme kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo mkoani humo.
Akitoa taarifa ya mkoa huo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani humo, Shigela amesema, hatua hiyo itapunguza gharama ya uzalishaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo na kuwawezesha kupata faida kubwa.
Shigela amesema, mbali na nishati kupelekwa kwa wachimbaji wadogo, serikali pia imepeleka umeme kwenye vijiji 485 kati ya vijiji 488 mkoani humo na hivyo baada ya muda mfupi wananchi wote wa mkoa huo watapata nishati ya umeme.
Kuhusu maonesho ya mwaka huu ya teknolojia ya madini, Shigela amesema, kumekuwa na ongezeko la waoneshaji 500 kulinganisha na mwaka jana 2023 ambapo kulikuwa na washiriki 317 na mwaka huu ni washiriki 817.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa