MWENYEKITI WA BODI YA EITI AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA TEITI (MSG)
Afurahishwa na utendaji kazi wao
Awataka TEITI kuendelea kuweka wazi Mikataba
Mwenyekiti wa bodi ya EITI Rt. Hon. Helen Clark leo tarehe 03 April 2024 akiendelea na ziara yake hapa nchini Tanzania akutana na wajumbe wa Kamati Tekelezi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia TEITI kwa lengo la kujifunza jinsi gani bodi ya wajumbe inavyofanya kazi katika nyanja mbalimbali kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unafanyika kikamilifu katika sekta ya uziduaji.
Akizungumza wakati wa Kikao hicho kinacholenga kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI CPA Ludovick Utouh alisema ujio huu wa Rt. Helen ni fursa kubwa sana katika utekelezaji na kusimamia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ya TEITI kulingana na Sheria ya TEITI (TEITA Act-2015) inavyoelekeza kuhakikisha TEITI inafikia katika viwango vikubwa vya Kimataifa.
Aidha, Rt. Helen Mwenyekiti wa Kamati bodi EITI aipongeza Kamati ya TEITI kwa kusimamia vema shughuli za Uwazi na Uwajibikaji katika sekta ya Uziduaji kuhakikisha mikataba inawekwa wazi na kuhakikisha TEITI inatekeleza shughuli zake kulingana na takwa la kisheria.
“Hatua hii ya kutaka kuweka wazi mikataba kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi na kimatiafa itasaidia TEITI kufanya vizuri katika kuyafikia malengo ya Taasisi na kuongeza ufanisi mkubwa, amesema Rt. Helen Clark. TEITI imekuwa mfano bora kwa kusimamia shughuli za TEITI kwa kutekeleza vigezo vya Kimataifa kama mpango wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uwazi, Uwajibikaji na Uhamasishaji (EITI) unavyoelekeza kwa nchi wanachama.
Nimevutiwa na Tanzania ambapo inaonekana kuwa nchi ya mfano mzuri katika usimamizi mzuri wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia pia kushukuru Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shughuli za Uwazi na Uwajibikaji katika sekta ya uziduaji sinafanywa kikamilifu na TEITI kufikia vigezo vya juu vya Kimataifa........

TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa