MWENYEKITI WA BODI YA EITI RT. HON HELEN CLARK AKUTANA NA ASASI YA KIJAMII HAKIRASILIMALI
Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Rt. Hon Helen Clark, amekutana na kufanya mazungumzo na jukwaa la Asasi za Kijamii ambazo zinashuhgulikia masuala ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini Tanzania – (Hakirasilmali) leo jijini Dar es salaam.
Ikiwa leo ni siku ya pili ya ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Rt. Helen Clark mategemeo ya ziara hiyo ni kuisaidia Tanzania kuimarisha usimamizi bora wa rasilimali zake za Madini, Mafuta pamoja na Gesi Asilia sambamba na kuisaidia Tanzania kufikia viwango vya Kimataifa katika usimamizi wa Uwazi na Uwajibikaji na kuendelea kuwa mfano kwa mataifa mengine katika usimamizi wa rasilimali hizo.
Rt. Helen Clark ameambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (TEITI) CPA. Ludovick Utouh, Kaimu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya TEITI.
Aidha, Katika kikao hicho Mhe. Helen Clark alishukuru sana kuwepo kwa Asasi ya Kijamii - Hakirasilimali kushirikiana na TEITI katika usimamizi mzima wa Uwazi na Uwajibikaji katika sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia kupitia wachimbaji wadogo na uwezeshaji wa fursa kwa wanawake kujikita katika Sekta ya Madini Mafuta na Gesi Asilia.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa