Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Rt. Hon Helen Clark afanya ziara nchini Tanzania*
Mwenyeki wa Bodi ya Asasi ya Kimataifa ya EITI Rt.Hon. Helen Clark amewasili nchini kwa ziara ya siku sita kuanzia tarehe 3-8 Aprili 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Bw. Kheri Mahimbali akiambatana na CPA. Ludovick Utouh ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI, Balozi Kaganda kutoka Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bi. Mariam Mgaya Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI walimpokea Rt.Hon.Helen Clark. Akiwa hapa nchini atakutana na wadau mbalimbali kujadili Utekelezaji wa shughuli za Uwazi na Uwajibikaji katika usimamizi wa Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia hapa nchini.
Aidha, tarehe 4 Aprili, 2024 atakutana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Wizara ya Madini.
Rt.Hon.Helen Clark alishakuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa nchi ya New Zealand na Mtendaji Mkuu wa UNDP.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa