Mwenyekiti wa vyama vya uchimbaji madini nchini (FEMATA), John Bina amesema tayari wamekaa na serikali na kukubalina kuendelea kuiuzia dhahabu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa silimia 20 kama ilivyopendekezwa awali.
Akitoa salamu za FEMATA wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya Kimataifa ya Teknoloji ya Madini, Bina amesema hapo awali kulikuwa na sintofahamu kati ya Serikali na wauzaji madini lakini baada ya kukutana na kuzungumza, sasa wamekubaliana kuwa Benki Kuu itanunua asilimia 20 ya dhahabu kutoka kwa wauzaji nchini.
Bina amesema, kulikuwa na tishio la mgomo kwa wauzaji wa madini lakini baada ya kukutana Ijumaa hii, mkoani Dodoma kila muuzaji amekubali kuiuzia BoT dhahabu kwa asilimia 20 na kuondosha athari ambazo zingejitokeza kama wasingekukubali kuuza dhahabu hizo.
Kuhusana na maendeleo ya sekta ya wachimbaji wadogo wa madini nchini, Bina amesema, mpaka sasa wanachangia asilimia 40 ya mapato ya dhahabu na kwamba wanatarajia kuongeza kiwango hicho na kuwazidi hata wachangiaji wakubwa
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa