Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wachimbaji hasa wadogo kuuza dhahabu zao Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili Tanzania iwe na akiba kubwa ya dhahabu na hivyo kuimarisha shilingi ya Tanzania.
Akihutubia wakati akifungua Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknoloji ya Madini, Dkt. Biteko amesema, mpango wa BoT kununua dhahabu ni kwa manufaa ya nchi lakini pia mchimbaji anaweza kunufaika na misamaha inayotolewa na Serikali.
Dkt. Biteko amesema, lengo la Serikali ni kuwa na akiba ya rasilimali hiyo ambayo kwa Afrika ni nchi ya nne kwa upatikanaji wa madini hivyo ni vyema kuweka akiba ya kutosha ya dhahabu ili kuilinda thamani ya shilingi ya Tanzania.
Kuhusiana na maonesho ya madini yanayoendelea, Dkt. Biteko amesema ni kielelezo muhimu kwa sekta ya madini na teknolojia zinazooneshwa katika maonesho hayo zinatoa nafuu kwa wachimbaji kupata zana za kisasa za kufanyia shughuli zao.
Amewataka wachimbaji wadogo kubadilisha mitazamo yao kwenye uchimbaji wa dhahabu na kutumia teknolojia hizo ili kuboresha uchimbaji wao na hivyo kupata tija kubwa kwenye rasilimali za dhahabu
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa