RAIS WA FEMATA AIPONGEZA TEITI KTK MAONESHO YA 48 YA SABASABA.
Leo tarehe 09 Julai, 2024 Rais wa Shirikikisho la vyama vya Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) John Bina ametembelea banda la TEITI na kutoa wito kuwa chama cha Wachimbaji wadogo ushirikiano kufanya kazi na TEITI, na kuipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa kazi nzuri ya kuwainua wachimbaji wadogo wa Madini.
Akipokea maelezo katika Banda la TEITI, alielezwa kuwa ripoti ya 14 ya TEITI iliyowekwa wazi mwezi Juni 2024 imeainisha takwimu na taarifa za wachimbaji wadogo hapa nchini. Aidha, Bina alisisitiza kuwa mlango wake upo wazi kushirikiana na TEITI ili kuhakikisha uwazi unaongezeka katika sekta hasa kwa wachimbaji wadogo.
Alisema wachimbaji wadogo wamekuwa wakichangia sana upande wa CSR lakini taarifa hizo hazifahamiki kwa jamii. Hivyo FEMATA ipo tayari kushirikiana na TEITI kuhakikisha mafanikio ya wachimbaji wadogo yanafahamika kwa wananchi.
TEITI inawakaribisha wanananchi wote wa Dar es salaam na maeneo ya karibu kutembelea katika banda la Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake katika maonesho ya sabasaba ili kujifunza namna ya kutumia takwimu zitolewazo na TEITI katika ripoti zake za kila mwaka. Ripoti ya 14 ya TEITI inapatikana katika tovuti ya TEITI. www.teiti.go.tz
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa