Sekretarieti Ya Umoja Wa Kimataifa Ya EITI Ya Nchini Norway Yawafunza TEITI
Mkurugenzi wa nchi wanachama wa EITI zinazoongea lugha za Kiingereza Afrika Bw. Gilbert Makore akutana na watumishi wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia TEITI leo tarehe 04 Novemba, 2024 Dodoma kwa lengo la kuwapitisha watumishi wa TEITI katika vigezo vipya vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya mwaka 2023 (EITI Standard 2023).
Akiongea na watumishi hao amewahasa kutekeleza matakwa ya Uwazi na Uwajibikaji kama ilivyoanishwa katika EITI Standard 2023. Ameeleza kuwa moja ya vipengele vilivyoongezeka ni pamoja na upingaji wa rushwa, masuala ya jinsia jamii na mazingira, muhamo wa nishati, uongezaji na ukusanyaji wa mapato katika Sekta Uziduaji. Pia amesisitiza watumishi wa TEITI kuzingatia na kutekeleza matakwa ya EITI kama inavyoelekezwa.
Aidha, akizungumzia kuhusu ushirikiano na uzoefu wa kikazi katika umoja huo wa kimataifa EITI, Bw. Makore ameeleza kwamba TEITI ina fursa kubwa ya kuendelea kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nhini Tanzania amesema utekelezaji wa shughuli za TEITI chini ya umoja wa Kimataifa EITI unazingatia miongozo ya EITI (EITI Standard).
Dhumuni kubwa la Tanzania kujiunga na Asasi ya EITI ilikuwa ni kuweka wazi taarifa za malipo na mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji Madini, Mafuta na Gesi Asilia; kwa kuweka wazi taarifa za malipo ni msingi mzuri wa kuboresha usimamizi na utawala bora katika uvunaji wa mali asili.
Hivyo upatikanaji wa taarifa za malipo na mapato inaongeza Uwajibikaji kwa Kampuni na Serikali na hivyo kupunguza mianya ya rushwa. Serikali inaweza kutumia EITI standard kama zana (Tool) ya kuainisha njia za kuboresha usimamizi wa sekta, kivutio cha wawekezaji, kuongeza mapato, na kujenga Utekelezaji wa EITI unasaidia kuweka mazingira mazuri ya mahusiano na jamii na hivyo kujenga taswira nzuri kwa kampuni uaminifu kwa wadau. Uwekaji wazi wa taarifa mbalimbali katika ripoti za TEITI zinasaidia Asasi za Kiraia kuhoji na kuwashirikisha wananchi juu ya Mchango wa Sekta ya Uziduaji nchini.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa