Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai azindua taarifa ya TEITI na Utoaji wa Leseni Kwa Kampuni ya Tembo Nickel Co. Ltd
Na Godwin Masabala Dodoma,
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua rasmi ripoti ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) ya kumi na moja (11) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na utoaji wa leseni kubwa kwa Kampuni ya Tembo Nickel Company Limited (Ltd).
Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dodoma tarehe 27 Oktoba, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kitwete Convention Centre kwa lengo la kuzindua ripoti ya kumi na moja (11) ya TEITI zoezi hili lilienda sambamba na utoaji wa Leseni Kubwa kwa Kampuni ya Tembo Nickel Co. Ltd. Halfa hiyo ilihudhuliwa na Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai pia na Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko, Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila,aliyekuwa Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Anne Semamba Makinda, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula, Mhandisi Yahya Samamba, Rais wa Kampuni Tembo Nickel Co. Ltd Bw. Chris Showalter, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI Bi Mariam Mgaya, Mwenyekiti wa Bodi ya TEITI Bw. Ludovick Utouh, pamoja viongozi mbalimbali.
Ripoti hiyo ya TEITI ya 11 inaonyesha jumla ya Tsh 623.16 bilioni zimepokelewa Serikalini katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa kampuni zililipa Tsh 626.14 bilioni chini ya kiasi ambacho Serikali imekiri kupokea. Alisema tofauti hiyo ni asilimia 0.48 ya mapato yote yaliyoripotiwa na Serikali.
Spika wa Bunge Job Ndugai alipongeza ripoti ya TEITI na kutoa wito wa kuangaliwa kwa sababu za kutofikishwa kwa asilimia 0.48 ya mapato ya wawekezaji kwenye sekta hiyo. Alisema tofauti inawezekana inatokana na upungufu katika uhasibu lakini akawataka wafanyie kazi ili ripoti ijayo iwe na mapato lingaifu kwa asilimia 100.
Kuhusu Leseni ya Nickel Kampuni ya Tembo Nickel Ndugai alitaka Wizara ya Madini kuangalia madini mengine yaliyopo Wilaya ya Ngara ili Taifa liweze kunufaika na madini yaliyopo. Alisema Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini itakuwa maco na mradi huo wa chombo hicho kwa niaba ya Bunge.
Aidha, aliwataka Watanzania ambao watakwenda kufanya kazi katika Kampuni Tembo Nickel Company Limited kulinda rasilimali za nchi.
Naye Waziri Biteko amesema kuwa mantiki ya falsafa ya Uwazi na Uwajibikaji kwenye Sekta ya uziduaji inatokana na Ibara ya 8 (1) (c) na Ibara 27 (1) & (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambapo ibara hizi zinazungumzia Serikali kuwajibika kwa wananchi wake na kuwa rasilimali zote za nchi zitatunzwa na wananchi wote kwa manufaa ya wote.
Imeleezwa kuwa, Tanzania ilijiunga katika mpango wa kimataifa wa kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Uchimbaji wa Rasilimali Madini mwaka 2009 lengo lake kuu ikiwa ni kuhakikisha kwamba mapato yanayotakiwa kulipwa Serikalini kutoka katika Sekta ya Uziduaji yanapatikana na yanawekwa wazi kwa wananchi.
Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko alisema mafanikio yanayotarajiwa kutokana na mradi huu ni kutengeneza ajira 978 na Tsh 17.35 trilioni sawa na Dola za Marekani bilioni 7.54.alisema mapato hayo yanatokana na gawio la hisa huru za Serikali, tozo na kodi mbalimbali zinzotokana na madini yatakayozalishwa kwa kipindi chote cha uhai wa mradi huo. Alisema kipindi hicho kitahitaji marighafi mbalimbali ikiwa ni pamoja na chokaa, magadi soda, sulphuric acid na hydrochloric acid zitakazochochea kukua na kuanzishwa kwa migodi mipya ya kuzalisha malighafi hizo.
Alisema manufaa mengine ni kukua kwa mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa, kuchochea ukuaji wa sektaa nyingine za kiuchumi kama viwanda, biashara na sekta za kifedha. Biteko alisema hadi Septemba 2021 leseni ambazo zimetolewa ni leseni 1,044 za utafutaji wa madini, leseni 15 za uchimbaji wa kati, leseni 161 za uchimbaji mdogo, leseni 1,561 za biashara ya madini. Alisema kwa leseni hizi pamoja na kuendelea kusimamia shughuli za uchimbaji, Serikali imeweza kupata mapato zaidi, akitoa mfano mwaka 2020/21 Wizara imekusanya Tsh 584.8 bilioni sawa na asilimia 111.03 ya lengo lililokuwapo la Tsh 524 bilioni. Biteko alisema wachimabaji wadogo wameweza kuchangia kwa asilimia 30 ya makusanyo yatokanayo na madini ya dhahabu
“Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati kabisa kuona kwamba Sekta ya Uziduaji inawanufaisha watanzania wote na wawekezaji kwa kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato yake stahiki na wananchi wanashiriki kikamilifu katika usimamizi wa rasilimali hizo,” alisema Waziri Biteko.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa