‘Tanzania itaendelea kutekeleza vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya Umoja wa Kimataifa - EITI kikamilifu’
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini-Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 25 Novemba 2022 alipokutana na Ujumbe kutoka EITI - Olso - Norway Bw. Gilbert Makore.
Katika Mkutano huo, Waziri Biteko alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kutekeleza kikamilifu masuala ya Uwazi na Uwajibikaji katika usimamizi wa Rasimimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa kuhakikisha kila mwaka TEITI inaweka wazi taarifa za malipo ya makampuni na mapato ya Serikali kupitia rasilimali hizo. Pia, Mhe. Waziri amesisitiza kuwa Umoja wa Kimataifa wa EITI kuzingatia masuala ya Mazingira kwenye sekta ya Uziduaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa masuala ya kimazingira ndani ya sekta hizo.
Aidha, Ujumbe kutoka EITI umepongeza Wizara ya Madini kwa kuendelea kusimamia shughuli za TEITI na kutekeleza vigezo vya Kimataifa vya EITI kimamilifu hata kwenda mbali zaidi katika utekelezaji wa Vigezo hivyo (implementing beyond the EITI Standard). Alisema “Tanzania imekuwa nchi ya mfano mzuri katika ripoti zake ukilinganishwa na nchi zingine wanachama, ni matumaini yangu kuwa tathmini itakayokufanyika Aprili, 2023 Tanzania itafanya vizuri zaidi.
Pia, katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Bw. Ludovick Utouh alimshukuru Waziri wa Madini kwa kazi nzuri zinazofanywa na Wizara yake kwa Ujumla pamoja na kuwezesha TEITI kupata Muundo wake na kuongezewa watumishi katika kuhakikisha kuwa TEITI sasa inajisimamia na kuweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa