TEITI KUWEKA WAZI RIPOTI YAKE YA MWAKA 2020/21 KABLA YA TAREHE 30 JUNI 2023.
Kamati ya TEITI imekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili maandalizi ya ripoti ya TEITI ya kumi na tatu (13) kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Kikao kazi hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Ludovick Utouh kimepokea matokeo ya ripoti hiyo yaliyowasilishwa na (IA – Independent Administrator) - Mtaalam elekezi M/s Chuo Kikuu Mzumbe.
Kulingana na matakwa ya Kimataifa ya EITI ripoti hiyo inatakiwa kuwekwa wazi kabla ya tarehe 30 Juni 2023.
Aidha, Mwenyekiti wa wa Kamati ya TEITI Bw. Ludovick Utouh aliwasisitiza wataalam elekezi kutoka (Chuo Kikuu Mzumbe) kukamilisha ripoti hiyo kikamilifu ndani ya mda.
Zifuatazo picha katika matukio:
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa