TEITI YAANIKA MATOKEO YA RIPOTI YA 14 YA TEITI
Kampuni 48 za Madini, Mafuta na Gesi Asilia pamoja na watoa huduma katika sekta yafanyiwa ulinganishi.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi kutoka TEITI Bw. Erick Ketagory katika Maonesho ya 48 ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es salaam. Akielezea washiriki alisema ' Ripoti hii imeandaliwa na Wataalam wa ndani wa Taasisi ya TEITI kwa mara ya kwanza tokea Taasisi hiyo ianzishwe'
Ripoti ya 14 ya TEITI imeonesha kuwa Serikali imepokea kiasi Shilingi trillion 1.878 kutoka kwenye Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia yaliyolinganishwa. Tofauti ya Malipo ya Kampuni na Mapato ya Serikali ni milioni 402 sawa na Asilimia 0.021 ya mapato yote yaliyopokelewa.
Aliongezea kwa kusema kuwa, pamoja taarifa za ulinganishi wa Malipo ya Makampuni na Mapato ya Serikali Ripoti hii ya TEITI imeweka taarifa na tawimu za Uzalishaji wa Madini mbalimbali hapa nchini pamoja na uzalishaji wa Gesi Asilia katika vituo vya Songosongo na Mnazi Bay.
Ripoti hii ya TEITI imetoa mapendezo saba (7) kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa Sekta ya uziduaji hapa nchini ili manufaa ya rasilimali hii yaongezeke kwa wananchi na nchi kwa ujumla.
Ripoti hii ipo wazi kwa matumizi ya Umma na inapatikana katika Tovuti ya TEITI www.teiti.go.tz
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa