TEITI yaaswa kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji na wadau mbalimbali
TEITI imeendelea kushiriki katika maonesho ya nne ya Teknolojia na uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika mkoani Geita. Leo Septemba 24, 2021 wadau mbalimbali waliotembelea Banda la Wizara ya Madini ambalo limeunganishwa na TEITI wameipongeza TEITI kwa kuendelea kuelimisha umma na kushauri kuwa TEITI iendelee kujitangaza kwa kuwa haijulikani kwa wananchi walio wengi.
Aidha, wananchi na wadau mbalimbali walipata fursa ya kufika katika banda letu wamepongeza na kufurahishwa na maonesho hayo vile vile wameitaka TEITI kuendelea kutumia vipindi vya redio na mitandao ya kijamii katika kuendelea kuelimisha umma na kuwafikia wananchi wengi zaidi juu ya shughuli zinazofanywa na Taasisi ya TEITI hasa hasa takwimu zinazopatikana kwenye ripoti zake ni za muhimu sana wananchi na wadau mbalimbali kufahamu zaidi juu ya michango kama (uhusishwaji wa huduma kwa jamii - CSR) inayofanywa na makampuni ya uchimbaji madini, mafuta na gesi asili na michango kama (service levy) inayoletwa kutokana na uchangiaji huo kutoka kwenye maeneo mbalimbali ambapo makampuni hayo yanafanya shughuli zao.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa