Mwandishi wetu Dar.
Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Godwin Masabala amesema kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa namna inavyotimiza majukumu yake ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa mujibu wa Sheria.
Ameyataja majukumu yao wanayoyasimamia kwa mujibu wa sheria ni pamoja na kuweka wazi taarifa za Mapato ya Serikali na malipo ya Kodi yanayotoka kwenye Kampuni za Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa Umma ili kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali hizo.
Masabala ameyasema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari yaliyofanyika Julai 11,2022 katika Banda lao lililopo ndani ya Banda kuu la STAMICO kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amefafanua kua Taasisi hiyo imeundwa kwa Sheria namba 23 ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeunda Kamati ya Uwazi na Uwajibikaji (Kamati ya TEITI) yenye wajumbe nane(8) na inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh na kazi za kila siku za TEITI zinatekelezwa na Katibu Mtendaji.
"Taasisi hii ina wajibu mkubwa wa kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia" amefafanua.
MWISHO
http://www.diramakini.co.tz/2022/07/teiti-yawaongezea-maarifa-wananchi.html
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa