*YALIYOJIRI WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MADINI NA UWEKEZAJI TANZANIA 2024, ULIOFANYIKA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE (JNICC), LEO NOVEMBA 19, 2024 JIJINI DAR ES SALAAM*
*Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan*
# Malengo mahususi ya mkutano huu ni kuvutia uwekezaji kutoka nje kuja nchini; kubadilishana maarifa na uzoefu mlionao katika Sekta ya Madini; kukuza usimamizi bora wa rasilimali tulizonazo za madini; kuongeza fursa za ajira na maendeleo ya jamii inayozunguka maeneo ya uchimbaji madini; kuimarisha ushirikiano kati ya serikali za nchi mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo katika tasnia ya madini.
# Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inaendelea kuongeza mchango wake, na hasa katika ukuaji wa uchumi wa nchi, kwa kuhakikisha kwamba sekta hii inachangia zaidi ya asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.
# Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekua, na kukua huku ni kutokana na ongezeko la asilimia 7.3 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9. Ni matumaini yangu kuwa ifikapo mwaka 2025 Sekta ya Madini itafikia lengo la mchango la asilimia 10 ya Pato la Ndani la Taifa.
# Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii serikali imechukua hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye Sekta ya Madini wanaendesha shughuli zao kwa tija kwa kuwezesha mazingira wezeshi ya uwekezaji na upatikanaji teknolojia unaimarika, hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo serikali imeamua kuimarisha kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuwezesha uwekezaji huo kuleta faida kwa kila mwekezaji.
# Kuongeza uwezo wa nishati ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, kuimarisha njia za usafirishaji kama vile barabara, reli, bandari na anga kwa kuongeza ndege na kujenga viwanja zaidi, yote haya ni kutaka kusaidia shughuli za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini kuweza kufanyika kwa tija lakini kuwapunguzia gharama wawekezaji.
# Serikali imesogeza huduma za masoko kila mkoa, na vituo vya kununulia madini katika maeneo ambayo madini yanachimbwa, na sasa tuna masoko 4
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa