WADAU WA MADINI WACHANGAMKIE FURSA SEKTA YA MADINI
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina amewataka wadau wa Sekta ya Madini kuchangamkia fursa zilizopo katika shughuli za uchimbaji madini.
Bina amesema hayo Mei 4, 2023 alipotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Kongamano la Wachimbaji wa Madini sambamba na Wiki ya Madini inayofanyika jijini Mwanza tarehe 3-10 Mei, 2023.
Pia, maonesho yamehudhuriwa na Taasisi mbalimbali za Serikali, Wizara ya Madini, Tume ya Madini, STAMICO, TEITI, TGC, Wachimbaji wadogo, Wafanyabiashara katika Sekta ya Madini na wadau mbalimbali wa Madini pamoja na Taasisi za Kibenki.
Kauli mbiu ya wiki ya Madini ni "Amani iliyopo Tanzania, itumike kuwa fursa kiuchumi na Tanzania kuwa kitovu cha Biashara ya Madini Afrika". Aidha Maonesho ya wiki ya Madini yamefunguliwa rasmi Mei 4, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa