WAJUMBE KAMATI YA TEITI WAITEMBELEA GGML - GEITA
Na Mwandishi wetu
Kamati ya wajumbe ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (TEITI) tarehe 16/02/2021 walipata fursa ya kutembelea Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold Mine Limited (GGML).
Kamati hiyo, iliongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Ludovick Utouh pamoja na Kaimu Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo Bi. Mariam Mgaya.
Utouh aliipongeza Kampuni ya Dhahabu ya GGML kwa kukubari kuruhusu kamati hiyo kutembelea Mgodi huo ikiwa ni moja ya sehemu ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uzalishaji, uchimbaji, utunzaji wa mazingira, ushilikishwaji wa jamii katika uchumi wa madini pamoja na uwajibikaji wa mgodi kwa jamii (CSR).
"Napenda kuchukua fursa hii kuupongeza Uongozi mzima wa mgodi wa GGML kwa kuafiki kamati hii kuja kujionea shughuli za uzalishaji unaofanyika katika mgodi huu, kiukweli tumejifunza mengi, hongereni sana," alisema Utouh.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa TEITI, Mariam Mgaya alisema, lengo la ziara hiyo ni kutaka kushuhudia shughuli za uzalishaji madini katika mgodi huo zinavyoendeshwa na kujionea uwekezaji ulivyofanyika katika mgodi huo.
Awali, Meneja Mahusiano wa GGML, Joseph Mangilima, alisema, Kampuni yao ndiyo inayoongoza kwa kuiingizia Serikali mapato ambapo mwaka ulioisha ulichangia katika halmashauri ya Mkoa wa Geita zaidi ya Sh. bilioni 9 ili isaidie katika masuala ya Kijamii (CSR).
Mgodi wa G
GML ulio gunduliwa mwishoni mwa miaka ya 1800 na kuanza rasmi uzalishaji mwaka 2009 umekuwa msaada mkubwa kwa wana Geita pamoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mangilima alisema, kwa sasa Mgodi huo unaendesha migodi mitatu ya chini kwa chini na mgodi mmoja wa wazi ambapo una wafanyakazi 2008 watanzania na 51 wangeni kati yao asilimia 11 ni wanawake na asilimia 89 ni wanaume na una kampuni mbalimbali zilizoajiliwa mgodini humo ambapo kuna zaidi ya watu 5000 wanaofanya kazi katika mgodi huo.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ziara hiyo kwenye mgodi wa GGML
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa