NAIBU Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya, amewataka wachimbaji wadogo-wadogo nchini kuachana na tabia ya kutorosha madini na badala yake wafanye shughuli zao kwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa ili kuiwezesha nchi kuongeza mapato.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa wachimbaji wadogo kwenye kikao cha kuhamasisha matumizi ya takwimu zinazotolewa taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini mafuta na geai asilia TEITI.
“Tuendelee kuwasihi wachimbaji wadogo kufanya maisha ya wizara inayowasimamia kuwa mepesi kwa kuacha kutorosha madini,” amesema Manya.
Aidha, mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Anna Rusambagula, ambaye ni Katibu wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Kagera (KAREMA), amesema wamefurahi kupata mafunzo hayo kutoka kwa watu wa TEITI.
“Mijadala yote imetugusa, kwani wizi unapotokea tunapunguza pato la taifa letu na kuwanyonya wachimbaji wakubwa wanaotegemea pesa kwa ajili ya madini kwani madini ni mali ya umma,” amesema Anna.
Hivyo tunawaomba mabenki watukopeshe ili tuweze kuendeleza pato letu na kuzuia watu wanaotoka nje ya nchi yetu wafaidi madini yetu kwa ajili ya mitaji yao mikubwa.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa