*WATUMISHI WANAWAKE TEITI WAADHIMISHA SIKU YAO DUNIANI*
*Waziri Gwajima atoa wito kwa Wanawake.*
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa Wanawake kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi nyingi kwa umakini na kwa uaminifu mkubwa.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Machi 8, 2024 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali II iliyopo Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
"Mwanamke ni Mama pia ni Kiongozi na ni mshauri mzuri katika jamii hivyo ni wasihi wanawake wenzangu tuendelea kuchapa kazi bila woga na tusichague kazi pia tusijihisi kwamba hatuwezi kufanya kazi fulani," amesema Dkt. Gwajima.
Kwa Upande wake Jacqueline Aloyce ambaye ni Kaimu Huduma wa Taasisi ya Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) amewataka wanawake wa Taasisi hiyo kuendelea kujitokeza kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuongeza mchango wa wanawake kwenye maendeleo ya Taifa na kusimamia Sheria ya TEITA Act ya mwaka 2015 na vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji EITI na kuhakikisha Miongozi na Taratibu zote za Serikali zinafuatwa.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yanafanyika jijini Dodoma ambayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo "Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii".
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa