WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO AMEKUTANA NA MABALOZI MBALIMBALI NA KUFANYA MAZUNGUMZO NAO.
Waziri wa Madini Doto Biteko leo tarehe 24/09/2019 amekutana na Mabalozi wa nchi mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Wa kwanza kukutana nae alikuwa Balozi wa Kenya Mhe. Dan Kazungu wakijadili masuala mbalimbali yahusuyo ushirikiano katika sekta ya Madini.
Baadae akafuata Balozi wa Uingereza, Sarah Cooke alie ambatana na mkuu wa Idara ya Sera, Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi huo, Bi. Laura Blizzard ( mwenye ushungi pichani).
Mwisho amekutana na Balozi wa Angola Sandro De Oliveira ambae alikuja kujitambulisha kwa Waziri wa Madini na Kuomba timu yake kutoka Angalo ije Tanzania kuja kuzungumza pamoja kuhusu masuala ya Mafuta sekta ambayo kwa Tanzania inasimamiwa na Wizara ya Nishati na baada ya mazungumzo Waziri alimuunganisha moja kwa moja na Waziri mwenye dhamana na Nishati.
Pamoja na mambo mengine Waziri amewaambia Mabalozi hao kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji wengi kwenye sekta ya Madini na kwamba wenye nia wote waje wizarani na kuachana na propaganda ya baadhi ya watu wasio itakia mema nchi wanaosemasema kuwa Tanzania hakuna mazingira rafiki ya uwekezaji.
Ameongeza kuwa yeye anapenda kuzungumzia mambo halisi (facts) na sio mambo ya kufikirisha hivyo amewaomba Mabalozi hao kwamba wawekezaji kutoka nchi zao kuja moja kwa moja Wizara ya Madini bila kupitia mikono ya watu wengine nje ya Wizara.
Waziri wa Madini kesho kutwa anategemea kuhudhuria Mkutano wa wawekezaji mkoani Lindi na baadae kuelekea Tunduru ambako atakuwa na Mkutano na wadau mbalimbali wa madini wakiwamo Wachimbaji wadogo
Wakati huo huo Waziri wa Madini atafanya mahojiano na Kituo cha Luninga cha ITV katika Studio za Dstv jijini Dar es Salaam na Kurushwa hewani siku ya Alhamisi katika vituo vya ITV na Dstv.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa