Serikali inapanga kununua helikopta kwa ajili ya uchunguzi wa madini nchi nzima ili kuwasaidia wachimbaji wadogo kutambua maeneo yenye madini na kuyafikia kwa urahisi.
Akitoa taarifa ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini, Waziri wa Wizara hiyo, Anthony Mavunde amesema, Serikali itanunua chopa hiyo itakayokuwa na uwezo wa kutambua madini yaliyopo ardhini kwa kina cha kilomita moja kutoka juu ya usawa wa ardhi.
Mavunde amsema, jitihada zote hizo zina lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kuchimba madini kwa uhakika na hivyo kuwawezesha kuyafikia madini bila kutumia gharama kubwa.
Amezitaja njia nyinginzo za kuwasaidia wachimbaji kuwa ni pamoja na kununua mitambo ya uchorongaji miamba ya madini na kuipeleka kwa wachimbaji huku mitambo mingine ikiwa ni kwa ajili ya vijana na akina mama.
TEITI Office Dodoma
Postal Address: S.L.P 361 Kikuyu Ave.
Telephone: +255688386546
Mobile: +255688386546
Email: info@teiti.go.tz
Haki Miliki ©2017 TEITI .Haki zote Zimehifandiwa