Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri Mkuu Kassim amekutana na ujumbe kutoka Korea Kusini uliojumuisha viongozi wa makampuni makubwa ya madini yanayohusika na mnyoyororo wa thamani wa uzalishaji betri za magari ya Posco Holdings, Posco International, SK, Korea Zinc na LX International.